Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha cha Shirika la Habari la Hawza, Hizbullah imetoa salamu za rambirambi kufuatia kufariki kwa Marji' mkubwa wa kidini, Ayatullah al-Udhma Sheikh Is'haq Fayyadh, na kusisitiza kwamba; alikuwa mmoja wa nguzo za Marjaiyya ya kidini huko Najaf Ashraf na mmoja wa nyuso mashuhuri zaidi za Hawza ya kielimu.
Hizbullah katika taarifa yake ilisisitiza kwamba; Ayatullah Fayyadh alitumia maisha yake matukufu katika kuutumikia Uislamu halisi wa Muhammadi, alikuwa ni shakhsia ya hali ya juu kielimu, kiroho na kifikra, na pia kupitia athari zake na tafiti zake za kielimu, kifiqhi na kiusuli, aliitajirisha maktaba ya Kiislamu.
Hizbullah ilitoa salamu zake za pole na rambirambi kutokana na msiba huu kwa Marji' mkuu, Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Hussein Sistani, Mar'ajii wakubwa, Hawza za kielimu, wanazuoni wa Umma wa Kiislamu, pamoja na familia ya marehemu, wanafunzi wake na wafuasi wake wa kidini.
Matini ya taarifa hiyo ni kama ifuatavyo:
"Kila anapofariki mwanachuoni, hutokea pengo katika Uislamu, pengo ambalo hakuna kitu kitakacholiziba hadi Siku ya Kiyama." (Imam Sadiq as)
Kwa kuridhika zaidi na hukumu na makadirio ya Mwenyezi Mungu, na kwa huzuni na masikitiko makubwa, Hizbullah imepokea habari ya kufariki kwa Marji' mkubwa wa kidini, Ayatullah al-Udhma Sheikh Is'haq Fayyadh, mmoja wa nguzo za Marjaiyya ya kidini ndani ya Najaf Ashraf na mmoja wa nyuso mashuhuri zaidi za Hawza ya kielimu; ambaye alitumia maisha yake matukufu katika kuutumikia Uislamu halisi wa Muhammadi, kueneza mafundisho ya Ahlul-Bayt (as) na kulea vizazi vya wanazuoni, watu wenye fadhila na wanaotafuta elimu za dini ambao walipeleka ujumbe wake wa kielimu na kimaadili katika pembe mbalimbali za ulimwengu wa Kiislamu.
Marehemu huyo mkubwa alikuwa na shakhsia ya hali ya juu kielimu, kiroho na kifikra, na alikuwa miongoni mwa wanafunzi mashuhuri zaidi wa Marji' mkubwa, Ayatullah al-Udhma Sayyid Abul-Qasim al-Khoei, kupitia maandiko na tafiti zake za kielimu, kifiqhi na kiusuli, aliitajirisha maktaba ya Kiislamu, na kwa maneno yake alidumisha maadili halisi ya Uislamu ambayo yamejengwa juu ya msingi wa hekima, wastani na uvumilivu, kwa miongo mingi alikuwa na mchango katika kumjenga mwanadamu mwenye imani na uelewa, vilevile, alijulikana kwa misimamo yake ya kimsingi na thabiti katika kusimama pamoja na masuala ya haki ya Umma na alikuwa mtetezi wa haki za waliodhulumiwa.
Tunatoa salamu zetu za dhati kabisa za rambirambi na pole kwa Marji' mkuu, Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Hussein Sistani (Mwenyezi Mungu aendelee kudumisha kivuli chake chenye baraka), Marajii wakubwa, Hawza za kielimu, wanazuoni wa Umma wa Kiislamu, familia ya marehemu, wanafunzi wake, wapenzi wake na wafuasi wake wa kidini, na tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amuweke katika rehema na radhi Zake pana, na aijaalie familia yake pamoja na wapenzi wake subira na utulivu.
Maoni yako